Ni time ya kuzipata #Goodnews za Bongo Flevani… baada ya Nikki wa Pili kuitambulisha single yake mpya ‘Baba Swalehe’ Ijumaa iliyopita, sasa ni zamu ya kichwa kingine kutoka WEUSI kuwasogezea mashabiki wake wa Tanzania na Africa flava mpya ya muziki wa Bongo Flava.
Miezi kadhaa iliyopita Joh Makini alidondoka pande za South Africa ambako alikutana na mkali mwengine wa muziki wa HipHop pande hizo, AKA na wawili hao wakaingia studio na kutengeneza wimbo ambao leo tarehe 10 November 2015 single hiyo itatambulishwa kwa mara ya kwanza kwenye MTV Base kama #SpankingNew!
Wimbo mpya wa Joh Makini unaitwa ‘Don’t Bother’ na unatambulishwa leo kwa mara ya kwanza kupitia kituo cha MTV Base saa 12 jioni (1800hrs EAT) saa za Africa Mashariki… Mtayarishaji wa ngoma hii mpya ni mtu wetu Nahreel kutoka The Industry huku Video Director wa wimbo huo akiwa Justin Campos wa Gorilla Films kutoka South Africa.
Mikono ya Justin Campos pia imehusika kwenye video kadhaa za wasanii hawa wa bongo flevani, Game ya Navy Kenzo, Nobody But Me na Never Ever ya Vanessa Mdee, Nusu Nusu ya Joh Makini na Looking For You latest hit single ya kwake Jux.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.