Kama hujawahi kukutana na kichwa cha habari kinamchomtaja Jumanne Kishimba, basi taarifa ikufikie kwamba kwenye list ya Wabunge wataowakilisha Dodoma kwenye Bunge la 11 na yeye yumo.
Jumanne Kishimba ni Mbunge mteule wa Jimbo la Kahama, lakini aliwahi kuandikwa pia kutokana na elimu yake ya darasa la saba !!
Amepatikana kwenye exclusive interview na reporter wa millardayo.com, akaanza na stori kuhusu safari yake Kisiasa ilikoanzia >>> ‘Nawashukuru sana wapiga Kura wa Kahama kwa kunichagua, nilijaribu mwaka 2000 wakati Jimbo la Msalala halijagawanywa lakini tulifutwa Wagombea wote wa CCM kulikuwa na rafu kidogo tulicheza. Toka mwaka 2000 sikuwahi kugombea mpaka mwaka huu 2015‘ >>> Jumanne Kishimba, Mbunge mteule Jimbo la Kahama.
Jumanne Kishimba aliwahi kuendelea kuiwaza Siasa baada ya kushindwa kwa mara ya kwanza? >>> ‘Imekuwa kwenye ndoto zangu kwa kuwa biashara na siasa ni kama mtu na ndugu yake, kulikuwa na mvutano mkubwa kwa kuwa elimu yangu ni darasa la saba lakini nina uzoefu wa kutembea sehemu nyingi na nimefanya kazi nyingi, ni vizuri kukawa na mchanganyiko wa wenzetu wenye elimu na sisi wenye uzoefu tukatatua changamoto pamoja Bungeni‘. >>>
Anazijua changamoto za wananchi wake? >>> ‘Wananchi wangu wanahitaji dawa, dispensary, maji, umeme.. ni vitu ambavyo elimu ya darasa la saba kwa Mbunge sio tatizo, Bungeni huendi kufanya operation kwamba unaweza kuua watu. Bungeni ninapeleka mawazo ya walionituma na kuongeza ya kwangu kwa kuwa una uzoefu‘. >>> Jumanne Kishimba.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.