Stori ninayotaka kukusogezea ni hii kutoka kwa msanii Mh.Temba amezungumza kwenye exclusive interview kuhusiana na Mkurugenzi wao Said Fella kutaka kuacha kuwaongoza mwaka 2013.
Akiongea na ripota wa millardayo.com alisema..’2013 Said Fella alitaka kuacha kutuongoza sisi kwenye muziki kwasababu alituambia kwamba anapata lawama nyingi sana kuhusu sisi kwa hiyo aendelee kuishi na familia lakini mimi nikamwambia hapana kwasababu akituacha lazima tutapoteza mwelekeo’ Temba
‘Mimi namuamini Fella ni mtu ambaye anaupeo kuliko mtu aliyesoma, kwa mimi ninavyoamini aliniambia kwamba alikuwa anapewa lawama eti anatupendelea katika muziki kwa hiyo alikuwa akipata lawama kibao kuhusu sisi lakini mwisho wa siku tukamweka katika mstari na mpaka sasa tuko naye’ – Temba
‘Hapa bado Saidi Fella alikuwa anatuongoza sisi kama TMK wakati huo wengine walikuwa wameshajitoa kama marehemu YP, Y Dash walijitoa kipindi hicho na wakaamua kuanzisha kundi lao sasa kibinadamu kugawanyika kwa makundi hayo ndio ilikuwa chanzo cha kumuumiza Said Fella’ – Temba
‘Kwa upande wangu kabla sijawa mwanamuziki mimi nilikuwa Askari nimeingia JKT nimetumikia jeshi miaka sita na mkataba ulipoisha ndipo nikaacha lakini pia nilikuwa nacheza Basketi baada ya hapo ndipo nikatoa single yangu ya kwanza’ – Temba