Imekuwa biashara ya kawaida kwa wasanii wa muziki kupromote ngoma zao kupita mitandao ya kijamii ili kutengeneza attention na hamu kwa mashabiki kupokea kile kipya kutoka kwao. Lakini kabla ya mitandao ya kijamii na YouTUBE kushika kasi, ulishawahi kuwaza mastaa walikuwa wanatumia njia gani kupromote kazi zao?
Nimekutana na interview moja ya staa wa muziki wa HipHop kutoka Marekani, Ja Rule ambaye miezi kadhaa iliyopita rapper huyo alipost picha kwenye page yake ya Instagram kuwakumbusha mashabiki moja ya vitu alivyowahi kugawa kama zawadi za promotion kwa ajili ya kuipromote kazi yake ya Thug Lovin moja ya ngoma kubwa sana za Ja Rule miaka ya 2000.
Kama ulikuwa hufahamu, Ja Rule aliwahi kugawa zawadi za condom zenye jina lake na jina la wimbo wake ‘Ja Rule: Thug Lovin’ kama njia nyingine ya kupromote ngoma yake mwaka 2002… na kwenye interview niliyokutana nayo Ja aligusia kwanini aliamua kugawa zawadi ya namna hiyo…
>>> “ Kipindi hicho wakati HipHop ilikuwa HipHop, tulikuwa tunatoa zawadi za kupromote kazi zetu kwenye radio, na kwa DJ’s ambao kwa asilimia kubwa walikuwa wanasaidia kutegeneza attention ya ngoma zetu kwa kuzipiga kwenye Club mbalimbali… sasa nilipoachia ngoma ya Thug Lovin, hiyo ilikuwa moja ya zawadi za promotion nilizokuwa nagawa, ‘Ja Rule: get your Thug Lovin’ condoms ili single yangu ichezwe…” <<< Ja Rule.
Kwa mujibu wa mtandao wa Complex, inasemekana kuwa wimbo wa Ja Rule, Thug Lovin ndio uliomrudisha Bobby Brown kwenye game baada ya kupotea kwenye headlines za muziki Marekani.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE