Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo.
Najua huenda stori nyingine zinakupita, hapa nimezikusanya zote zilizoguswa na #Tweets za #Magazeti November 17, 2015, unazisoma zote kwa pamoja.
Rais JPM amepiga marufuku wasaidizi wake kupokea zawadi kutoka kwa mtu au taasisi kwa ajili ya Rais #GazetiCHANGAMOTO #NOVEMBER17
— millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Wafanyabiashara soko la Sabasaba Dodoma wamelalamikia kukosa wateja kutokana na Manispaa kutozoa taka kwenye soko hilo #CHANGAMOTO — millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Baadhi ya wajawazito Chamwino Dodoma wamelalamikia kutozwa faini ya 20,000 na wahudumu wa afya ikitokea wamejifungulia nyumbani #CHANGAMOTO
— millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Rais JPM ‘atua’ Bandarini, mita za mafuta za Mabilioni zafungwa, ‘pepo’ la ukwepaji wa Kodi lafikia tamati #GazetiJAMHURI #NOVEMBER17 — millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Dk. Tulia ACKSON ateuliwa kuwa Mbunge na kuwania Unaibu Spika, ni Mbunge wa kwanza kuteuliwa na Rais JPM #UHURU >>https://t.co/dyHSGRAHok
— millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Halmashauri ya Manispaa Temeke imesema ‘bomoa bomoa’ ya Shimo la Udongo Kurasini upo kihalali, wananchi wamelipwa fidia #UHURU #NOV17 — millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Serikali Mkoa wa K’njaro imeingia Mkataba na Halmashauri, watendaji watakaoshindwa kusimamia usafi kufukuzwa kazi #GazetiUHURU #NOVEMBER17
— millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Hospitali ya Muhimbili imesitisha huduma ya kipimo cha MRI baada ya kuharibika tena, imefanya kazi kwa siku mbili tangu itengenezwe #UHURU — millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Mvua yazua kizaazaa Tanga, wanafunzi walazimika kurudi nyumbani baada ya madarasa kujaa maji #GazetiUHURU #NOV17 >>https://t.co/dyHSGRAHok
— millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Mahakama Kuu kanda ya Dodoma imemhukumu kunyongwa mpaka kufa mtu mmoja baada ya kukutwa na hatia ya kuua kwa kukusudia #GazetiUHURU #NOV17 — millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Mtu mmoja ameuawa kwa kukatwakatwa na watu wasiofahamika Sumbawanga, chanzo chadaiwa ni wivu wa mapenzi #RaiaTZ >>https://t.co/dyHSGRAHok
— millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Baraza la mitihani limetangaza kwamba wanafunzi watakaofeli kidato cha pili hawatarudia darasa bali wataandaliwa utaratibu maalum #MWANANCHI — millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Mzee wa miaka 70 K’njaro anatuhumiwa kumuua mkewe na watoto wake wawili wadogo kwa kuwakatakata kwa panga na shoka #MWANANCHI #NOV17
— millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Wachimbaji watano wa madini kati ya sita waliodhaniwa wamekufa baada ya kufukiwa na kifusi kwa siku 41 wamekutwa hai huko Kahama #MWANANCHI — millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Mkurugenzi wa mashtaka amepinga kupewa dhamana kwa mtuhumiwa wa kesi ya MWAMUNYANGE, ni yule aliyesambaza taarifa za uongo #MWANANCHI #NOV17
— millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Mamlaka ya bandari Tanzania ipo ktk hatua za kurasimisha utaratibu wa kupima ulevi kwa wafanyakazi na wageni wanaoingia bandarini #MWANANCHI — millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Wakazi wa Kurasini, Dar wameilalamikia Serikali kuhusu kubomoa makazi yao na kutaka walipwe fedha halisi walizoahidiwa #MWANANCHI #NOV17
— millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Majaji na mahakimu kote nchini wameagizwa kumaliza kesi zote zinazohusiana na uchaguzi mkuu wa Oktoba25, ifikapo Machi 2016 #MWANANCHI NOV17 — millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Dr.Tulia Ackson huenda akawa mmoja wa Watanzania wachache wenye bahati ya kupata vyeo tofauti nchini ndani ya siku 67 #MWANANCHI #NOV17
— millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Mwingine auawa Geita huku kifo chake kikiwa cha kutatanisha, yadaiwa huenda ni kutokana na chuki za kisiasa zinazoendelea #MWANANCHI #NOV17 — millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Kasi ya Rais Dk.Magufuli imeanza kuwatoa jasho watumishi wa Serikali Geita, Ni agizo la kutaka watendaji kutatua kero za wananchi #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Ofisa mtendaji wa kijiji cha Nguriti, Tabora anadaiwa kuuza ng’ombe wawili waliotolea na rais mstaafu JK kwa ajili ya kikundi #MWANANCHI NOV — millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Uganda yaanza kuchukua tahadhari dhidi ya ugaidi,Jeshi limeimarisha ulinzi maeneo yote ya nchi kufuatia mashambulio yanayoendelea #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Lionel Messi anataka kitita cha paundi 600,000 kwa wiki kwa timu ambayo itataka kumsajili acheze katika ligi kuu ya England #MWANANCHI NOV17 — millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Cristiano Ronaldo atacheza mchezo wake wa mwisho wa El Clasico J’mosi huku kukiwa na taarifa kuwa ataondoka Real Madrid Mei 2016 #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Msafara wa Taifa stars umegoma kutumia basi waliloandaliwa na wenyeji wao Algeria kwa hofu ya hujuma baada ya kuwasili #MWANANCHI #NOV17 — millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Uwanja wa Simba uliopo Bunju B umevamiwa na baadhi ya watu walioanza kugawana maeneo tayari kwa ujenzi wa makazi #MWANANCHI #NOV17
— millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Mazungumzo ya kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa uchaguzi mkuu Z’bar yameendelea kwa mara ya tatu na kuonyesha mwelekeo mzuri #NIPASHE #NOV17 — millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Makamu wa Rais Samia Suluhu amewaomba viongozi wa dini kuendelea kuiombea Serikali ya awamu ya tano pamoja na uchaguzi Z’bar #NIPASHE #NOV17
— millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Idadi ya wagonjwa wa Kipindupindu waliolazwa katika vituo mbalimbali vya kuhudumia wagonjwa nchini hadi jana wamefikia 137 #NIPASHE #NOV17 — millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Kijana wa miaka 18 amefariki baada ya kupigwa na radi wakati akichunga ng’ombe,pia radi hiyo ilisababisha vifo vya ng’ombe 22 #NIPASHE NOV17
— millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Ahadi ya elimu bure iliyoahidiwa na Rais Dk.Magufuli inatishiwa na utitiri wa michango inayoendelea kutozwa ktk shule mbalimbali #NIPASHE — millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali imesababisha hasara kubwa baada ya kuezua nyumba 26, shule moja na makanisa mawili Mbeya #NIPASHE
— millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Job ndugai amejitabiria magumu katika bunge la 11 kwa kueleza kuwa litakuwa na changamoto nyingi ambazo atahakikisha anazimudu #NIPASHE NOV — millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Kipindupindu chaua mwanafunzi wa darasa la kwanza Lindi na watu wengine 54 wamelazwa kutokana na kuugua ugonjwa huo #NIPASHE #NOV17
— millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Askofu wa kanisa la RPCT amewataka maadui wanaomzunguka Rais Dk.Magufuli washindwe na kumwacha aendelee na kazi aliyoianza #MAJIRA #NOV17 — millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
TAKUKURU imewafikisha maofisa wawili wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa kutumia vibaya madaraka yao wakiwa watumishi wa umma #MAJIRA NOV
— millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Baraza la vijana CHADEMA limetoa siku 3 kwa Jeshi la Polisi kuwakamata waliohusika na mauaji ya M’kiti wa chama hicho Geita #MAJIRA #NOV17 — millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Wananchi Mwanza wamelalamikia kupanda kwa bei ya vyakula na kusababisha baadhi ya familia kula mlo mmoja kwa siku #MAJIRA #NOV17
— millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Hospitali ya rufaa KCMC inahitaji zaidi ya milioni 100 kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya maji na vyoo vya wodi za wagonjwa #MAJIRA — millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Mshambuliaji wa Tanzania Mbwana Samatta amegeuka kivutio kikubwa Algeria tangu afike kwa ajili ya mchezo wa marudiano #MAJIRA #NOV17
— millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Yanga imekana taarifa zilizoenezwa na watu kuwa wana mpango wa kumsajili mshambuliaji wa stand united Elias Maguli #MAJIRA #NOV17 — millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Nahodha wa Taifa Stars Cannavaro amesema leo watafia uwanjani dhidi ya Algeria ktk mechi ya marudiano ya kufuzu kombe la dunia #HabariLEO
— millard ayo (@millardayo) November 17, 2015
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokeamatukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE