Ernest Napoleon ni Mtanzania ambaye aliamua afanye kitu tofauti na kikubwa sana kwenye soko la movie Tanzania, aliweka nguvu yake, muda wake na pesa ya kutosha kuhakikisha anafanya movie kali ambayo itamgusa kila mtu.
‘Going Bongo‘ ndio movie yenyewe ambayo ina stori ya kuvutia sana.. Ernest mwenyewe aliwahi kufika studio za Millard Ayo na kufanya exclusive story kali kabisa kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa mikakati yake kuisuka movie hiyo mpaka ikakamilika.
Good News TANZANIA !! Going Bongo ilifanyiwa uzinduzi Tanzania na Uingereza na mastaa kibao wa Uingereza walikuwa sehemu ya wageni walioshuhudia uzinduzi huo… muda mfupi baadae Filamu hiyo tayari ina ushindi wa Tuzo mbili, Best East African Film iliyoshinda kwenye Tamasha la ZIFF Zanzibar, na pia Best International Film ambayo ilishinda kwenye Tuzo za BEFFTA za Uingereza.
Sasahivi ni zamu ya Tanzania, hii movie ilikuwa sokoni tayari lakini najua kuna watu wangu bado hawajaiona na wengine hawajajua kama ipo.. kwa time yako na watu wako mtaishuhudia LIVE kwenye screen kubwa ya Century Cinemax pale Mlimani City Dar es Salaam… hiyo itakuwa December 11 mwaka huu huu 2015.
https://www.youtube.com/watch?v=CcJXvuW4KtU&feature=youtu.be
Kipande kingine cha trailer ya movie hiyo hiki hapa.
https://www.youtube.com/watch?v=So0QIUM6kOM
Najua kuna aina ya stori kwenye movie zinajirudia na zimekuchosha, kama ungependa kuona kitu tofauti na kizuri unaweza kuicheki hii mtu wangu !! Kama ulipitwa na ile Interview pia unaweza kucheki hapa Ernest on AIR with Millard Ayo.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.