Jukwaa la Katiba leo limekutana na wanahabari Dar es salaam na kuzungumzia mambo mbalimbali yanayohusu uchaguzi mkuu uliomalizika pamoja na mchakato wa katiba mpya.
Mkurugenzi wa Jukwaa hilo Deus Kibamba amezungumza na kusema kuwa mchakato wa kuandika katiba mpya ulianza na Rais mstaafu Jakaya Kikwete , lakini baada ya Rais wa sasa wa awamu ya tano Dk.John Magufuli kuunda baraza lake la mawaziri na safu nzima ya uongozi anapaswa atekeleze ili kurudisha mchakato wa katiba na kuliwezesha taifa kupata katiba mpya na ya kidemokrasia.
“Ni wakati muafaka wa rais wa sasa Dk.Magufuli kulitangazia Taifa namna ya kurejea kwenye mchakato, kwa sasa hatma ya mchakato wa katiba haijulikani na ni vyema rais atumie mamlaka yake kuonyesha jinsi ya kupatikana kwa katiba hiyo ili Watanzania wapate katiba mpya na ya kidemokrasia”…Deus Kibamba.
Pia mara baada ya kupatikana kwa baraza la Mawaziri ni vyema Rais aelekeze Serikali kuanza kuandaa miswada kwa ajili ya marekebisho ya sheria mbili zinazoongoza mchakato wa katiba tayari kwa uwasilishaji Bungeni katika kikao cha pili kitakachofanyika Februari 2016.
Kingine kilichosikika kutoka ndani ya jukwaa hilo la katiba ni pamoja na mgogoro wa kisiasa unaendelea visiwani Zanzibar...Kitendo cha kufutwa kwa uchaguzi Zanzibar kimeibua mvutano mkali kati ya wafuasi na viongozi wa vyama vya siasa kiasi cha kusababisha sintofahamu na makundi..Rais aweze kuongoza jitihada za kuinusuru Zanzibar kuingia kwenye machafuko ya kisiasa”...Deus Kibamba
Jukwaa la katiba pia halikusita kumpongeza Dk. Magufuli kwa kusitisha safari za nje kwa viongozi na ziara za kushtukiza ..“Kwa kuwa rais ametambua kasoro zilizopo kwenye utaratibu mzima wa safari za nje, sisi tunamuunga mkono na kupendekeza kuwa utaratibu uainishwe mapema ili kuruhusu safari zenye maslahi mapana kwa Taifa tu”..pia wale watumishi wa umma wanaokutwa na makosa ni vyema wakasimamishwa kazi wanapokutwa na makosa kupisha uchunguzi na si kuhamishwa ofisi moja kwenda nyingine”.…Deus Kibamba
Jukwaa hilo pia limetoa maoni kwa Rais ahakikishe kuwa katika vipaumbele vyake na Serikali yake mchakato wa katiba mpya uwe kipaumbele cha kwanza ili kuweza kupatikana mapema.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokeamatukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayokwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.