Headlines kwa siku ya November 18 ni juu ya nani atakuwa waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli November 19 kupendekeza jina la waziri mkuu Kassim Majaliwa Kassim ambaye ataapishwa Ijumaa ya November 20 Dodoma.
Kassim Majaliwa ambaye ni mbunge wa Ruangwa sio jina geni katika medani za soka, kama unakumbuka vizuri Kassim Majaliwa aliwahi kuwa kocha wa mpira wa miguu na aliwahi kuifundisha klabu ya Singida United, kazi ya ukocha kwa waziri mkuu huyo haikuwa ya kubahatisha bali alikuwa akitambulika rasmi kama kocha mwenye leseni daraja B na shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika (CAF).
Afisa habari wa Azam FC Jafari Iddi Maganga amezungumzia na kumpongeza Mh Kassim Majaliwa
“Uongozi wa Azam FC na bodi ya uongozi ya Azam FC inampogeza Kassim Majaliwa kwa kuteuliwa kuwa waziri mkuu mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini kwa wale ambao hawafahamu Mh Majaliwa aliwahi kuwa kocha wa klabu ya Singida United miaka ya nyuma ana leseni B ya ukocha kutoka kwa shirikisho la soka barani Afrika CAF hivyo tumefuraishwa kwa yeye kushika nafasi hiyo” >>> Jafari Iddi
Msikilize hapa Jafari Iddi akimzungumzia Mh waziri Mkuu Majaliwa
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.