Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amelihutubia Bunge leo November 20 2015 Dodoma kwa mara ya kwanza tangu ameapishwa kuwa Rais wa awamu ya tano.
Hapa ninazo nukuu chache nilizozipata nikazisogeza kwenye #Tweets wakati wa hotuba yake.
Rais MAGUFULI # Maeneo yanayolalamikiwa kwa rushwa ni mengi,TAMISEMI kwa ubadhirifu wa fedha za umma, bandari,TANESCO,TRA #MillardAyoUPDATES
— millard ayo (@millardayo) November 20, 2015
Rais MAGUFULI #Inanibidi haya yote niyataje ili nijue tunaanzia wapi na tunakwenda wapi, nisipoyataja nitakuwa mnafiki -MillardAyoUPDATES — millard ayo (@millardayo) November 20, 2015
Rais MAGUFULI #Maeneo mengine yanayolalamikiwa ni Polisi, hospitali, mizani, mahakama, maliasili, vilio vya wachimbaji -MillardAyoUPDATES
— millard ayo (@millardayo) November 20, 2015
Rais MAGUFULI #Viko viwanda vingine wanafugia mbuzi wakati walipewa kwa madhumuni ya kuviendeleza, tutavichukua haraka -MillardAyoUPDATES — millard ayo (@millardayo) November 20, 2015
Rais MAGUFULI #Kodi ambazo hatuzikusanywi ni nyingi, niwatake viongozi walisimamie hili ikiwemo kutenga maeneo maalum -MillardAyoUPDATES
— millard ayo (@millardayo) November 20, 2015
Rais MAGUFULI #Kuanzia January ninaposema elimu bure namaanisha bure, na sio waanze kuweka michango ya ajabu ajabu -MillardAyoUPDATES — millard ayo (@millardayo) November 20, 2015
Rais MAGUFULI #Mimi nimewaahidi wananchi wangu kwamba nitapambana na rushwa na ufisadi bila haya kwa mtu yeyote -MillardAyoUPDATES
— millard ayo (@millardayo) November 20, 2015
Rais MAGUFULI #Nimeahidi kuunda mahakama ya rushwa na ufisadi,naamini hawataniangusha katika hili, sitakuwa na kigugumizi -MillardAyoUPDATES — millard ayo (@millardayo) November 20, 2015
Rais MAGUFULI #Nataka iwe ‘Kazi tu’ hatuwezi kulea watu ambao wanalipwa mishahara tu wakati hawafanyi kazi yoyote -MillardAyoUPDATES
— millard ayo (@millardayo) November 20, 2015
Rais MAGUFULI- Wizara zilizoongoza kwa safari za nje ni pamoja na Bunge, Ofisi ya Waziri mkuu, Wizara ya mambo ya nje…-MillardAyoUPDATES — millard ayo (@millardayo) November 20, 2015
Rais MAGUFULI- Kuna watu hapa wamesafiri kwenda nje kuliko hata wanavyokwenda kumsalimia baba na mama yake huko kijijini -MillardAyoUPDATES
— millard ayo (@millardayo) November 20, 2015
Rais MAGUFULI -Mmeshuhudia wenyewe kilichotokea leo hapa, bado tuna watoto wengi, tuendelee kuwavumilia na kuwafundisha -MillardAyoUPDATES — millard ayo (@millardayo) November 20, 2015
#MillardAyoUPDATES #RaisMAGUFULI #Bungeni kuhusu Wafanyakazi wa wizara wanaofanyia mikutano hotelini. pic.twitter.com/loWxlutfCw
— millard ayo (@millardayo) November 20, 2015
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayokwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.