Michezo

Hamad Ndikumana wa Irene Uwoya kakataliwa na kocha wa timu hii ya Ligi Kuu TZ, sababu ni hii …

on

Mwanasoka wa zamani wa timu ya taifa ya Rwanda na klabu ya Rayon Sports ya Rwanda Hamad Ndikumana amerudi tena katika headlines za soka November 20, Ndikumana ambaye ni mume wa muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya ametemwa na klabu yake ya Stand United baada ya kocha wa timu hiyo mfaransa Patrick Liewig kutohitaji huduma yake.

a1

Ndikumana ambaye alikuwa na klabu ya Stand United ya Shinyanga kwa kipindi cha miezi minne ametemwa rasmi na klabu hiyo, hivyo kwa sasa ni mchezaji huru, awali Ndikumana aliwahi kugoma kuichezea klabu hiyo baada ya kutomaliziwa malipo yake lakini msemaji wa Stand United ya Shinyanga Deokaji Makomba amethibitisha kuwa moja kati ya sababu zilizofanya wamuache staa huyo ni umri wake kuwa mkubwa.

Manchester City's Brazilian forward Elano (L) fights for the ball with AC Omonia's Rwandan defender Hamad Ndikumana during their UEFA Cup first round, second leg football match at the City of Manchester stadium, Manchester, north-west England, on October 2, 2008.  AFP PHOTO/ANDREW YATES (Photo credit should read ANDREW YATES/AFP/Getty Images)

Elano wa Man City akiwania mpira na Hamad Ndikumana wakati akiichezea AC Omonia hii ilikuwa ni moja kati ya michezo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

“Kocha amesema hatomuhitaji tena katika kikosi chake sababu kubwa ilitajwa na mwalimu ya kumuacha Hamad Ndikumana ni kuwa na umri mkubwa hivyo mwalimu kaona aachane nae kwani itakuwa ngumu kuendelea nae, Hamad Ndikumana hatupo nae tena na tayari ameshakamilishiwa haki zake” >>> Deokaji Makomba

Ndikumana ambaye amewahi kutamba na vilabu kadhaa anatajwa kuwa na umri wa miaka 37, umri ambao ni mkubwa kisoka, kama utakuwa unakumbuka vizuri Ndikumana ndio jamaa ambaye alimuoa mrembo kutoka kiwanda cha filamu za Kibongo Irene Uwoya na kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume anaitwa Krish.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments