Kazi mpya kutoka kwa Joh Makini sasa hivi ni audio na video ya Don’t Bother ambayo amefanya na A.K.A wa South Africa. Baada ya kufanya vizuri kwenye vituo mbalimbali vya TV na radio, hii ni nafasi yako kujua vitu 6 kutoka kwa Joh Makini mwenyewe ambavyo labda ulikua hivijui kuhusu audio na video ya Don’t Bother.
1)Don’t Bother ni video ambayo ilikua na location nyingi sana kati ya video zote za Joh Makini na director alilazimisha wa shoot kwenye location zote walizopanga. Walitumia siku mbili na nusu kumaliza video nzima
2)Kuna scene ambayo msanii A.K.A anarukia sofa ambalo lilikua linavutwa na gari, Joh anasema kwamba ilimchukua mara 3 msanii A.K.A kurukia na kuendelea kuchana mistari yake kwenye scene ile. Pia Joh Makini na yeye alidondoka wakati dereva anakata kona na kuingia kwenye shimo dogo ambalo lilifanya adondoke chini japokua aliweza kuendelea na shooting.
3)A.K.A alikua mwepesi sana kuelewa mistari ya kiswahili na kui-rap kwenye ile ngoma. Tofauti na walivyotegemea lakini A.K.A aliweza ku-flow vizuri kwa haraka sana japokua ilikua ni mara yake ya kwanza.
4)Ngoma ya Don’t Bother Joh Makini alikua ameshairekodi zamani sana na original version alikua peke yake. Baada ya kupata nafasi ya collabo na A.K.A akaichagua hiyo na kufuta verse moja na kumuachia A.K.A aichane verse yake.
5)Location inayoonekana kama wapo China ni kwamba walienda location moja huko Johannesburg inaitwa China Town wanaishi wachina wengi. Huko kuna majengo kama ya kwao China kwa hiyo unaweza kusema wame-shoot nchini China.
6)Ngoma ya Don’t Bother ili rekodiwa saa 11 asubui baada ya kwenda studio saa 4 usiku, muda wote huo walikua wanasubiri A.K.A amalize kurekodi ngoma yake na Diamond.