Hii stori nilikuzogezea muda mfupi uliopita kuhusu ishu ya mgomo wa wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha URAFIKI kilichopo eneo la Shekilango Dar es Salaam.
Updates za taarifa iliyonifikia muda mfupi uliopita ni kwamba Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, DC Paul Makonda ameagiza shughuli zote za kiwanda hicho zisimame kwa sasa mpaka mgogoro wa kimaslahi kati ya wafanyakazi na wamiliki wa kiwanda hicho utakapotatuliwa.
Hapa nanukuu maneno ya DC Paul Makonda mbele ya wafanyakazi hao >>> “Kwanza wasimamishe shughuli za uzalishaj, hatuwezi kuzalisha kwenye mazingira ambayo hayana amani… ninaenda kumtafuta Katibu Mkuu wa Wizara ili achukue hatua dhidi ya watawala wasio na majibu ya kero za wananchi“-
Sauti ya stori hiyo hii hapa kutoka kwenye habari ya TBC 1
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanzekupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.