Umaarufu wa staa wa movie Lupita Nyong’o unazidi kushika kasi kila mwaka, baada ya kutokea kwenye majarida mbalimbali kwa mwaka huu wa 2015, staa huyo wa movie mwenye asili ya Kenya amepata shavu la kufunga mwaka kwa kutokea kwenye jarida la Elle Magazine UK la Uingereza.
Jarida la Elle Magazine UK litakuwa sokoni mwezi January 2016, na humo ndani Lupita kagusia vitu vingi lakini haya ni mambo manne niliyofanikiwa kuyanasa kutoka kwa staa huyo wa movie za Hollywood.
Ulijisikiaje kucheza movie ya Star Wars: “Fursa ya kucheza movie hiyo ilinipa fursa ya kujaribu vitu vingi vinavyogusa uwezo wangu wa kuigiza… imenipa experience ya tofauti kabisa ukizingatia nimecheza nipo kwenye sayari nyingine ya tofauti sana“.
Unachukuliaje kuwa tofauti: “Ukiwasha TV na ukikutana na vitu ambavyo havikuwakilishi wewe basi inapoteza imani na mtu binafsi aliye ndani yako. Binafsi ilikuwa nikitazama movie za Hollywood sioni kitu kinachowakilisha vile nilivyo mimi… lakini badaaye nikakubali kuwa nipo kwenye jamii ambayo pengine haithamini sana rangi kama yangu“.
Umeshawahi kuishi kuhofia usalama wako?: “[Kuishi Mexico nikiwa mtoto] watu walikuwa wakituona wanatusimamisha kuomba kupiga picha na sisi kwa sababu tu tulikuwa watu weusi. Na wakati huwo ndio ujana umekolea, unajaribu kujitambua wewe ni nani na upo wapi huku ukijaribu kutengeneza njia yako mwenyewe ya maisha. Kilikuwa kipindi kigumu sana“.
Unachukuliaje umaarufu: “Sidhani kama tunatakiwa kupagawa sana na hali kama hii ya kimaisha. Natamani kungekuwa na switch ya kuwasha na kuzima kupunguza na kuongeza vitu maishani. Lakini kwa hali yangu nafanya maamuzi ya kina sana ya nini nataka kufanya, wapi na kivipi lakini kikubwa zaidi na nani“.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.