Beyonce amekuwa msanii ambaye wasichana wengi wanatamani kuja kuwa kama yeye siku moja, ushawishi wake umegusa watu wengi na sehemu mbalimbali duniani. Naamini kuna matukio mengi sana ya Beyonce ambayo tayari yameshagusa masikio yako na pengine unatamani kujua kitu kimoja tofauti kuhusu staa huyo.
Kama wewe ni miongoni ya watu ambao ni mashabiki wakubwa wa Beyonce Knowles basi hii inakuhusu moja kwa moja… nimefanya jitihada za kukusanya vitu mbalimbali ambavyo inawezekana wengi wetu hatuvijui kuhusu staa huyu wa muziki.
Hivi ni baadhi ya vitu sita vya kufahamu kuhusu Beyonce Knowles:
1 Beyonce alianza kuimba sauti ya kwanza akiwa na miaka nane.
2 Jina la ‘Beyonce’ ni jina la familia linalopewa kwa kila mtoto wa kwanza wa kike, na staa huyo alipozaliwa alirithi jina hilo kutoka kwa mama yake.
3 Mwaka 2011 Beyonce alitajwa na Guiness World Records kama mtu aliyeandikwa zaidi duniani kwa sekunde moja kwenye mtandao wa Twitter ambapo staa huyo alitajwa kwenye tweets 8868 baada ya kuitangazia dunia kuwa ana ujauzito wa mtoto wake wa kwanza, Blue Ivy.
4 Wimbo wa ‘Bootylicious’ ulioimbwa na kundi la Destiny’s Child (kundi la zamani la Beyonce) ulipata umaarufu mkubwa kitendo kilichopelekea neno hilo kutafsiriwa mwaka 2004 na kuwekwa kwenye kamusi ya Oxfrod Dictionary, na sasa neno ‘Bootylicious’ kwenye tafsiri ya kamusi humaanisha: >>> “(of a woman) sexually attractive especially women with curvaceous buttocks”. <<<
5 Album yake ya kwanza kama solo artist ya mwaka 2003, ‘Dangerously In Love’ ilikataliwa na lebo iliyokuwa inamsimamia (Colombia Records) kwa madai ya kuwa album hiyo haikuwa na nyimbo zozote ambazo ni hit songs… bila kujali Beyonce akaitoa album hiyo na badaaye ikaja kumuweka Beyonce kwenye chati na hizi 5 kali zilizokuwa zinapatikana ndani ya album hiyo; ‘Dangerously In Love’, ‘Naughty Girl’, ‘Me, Myself and I’, ‘Baby Boy’ na ‘Crazy In Love’.