Sean Paul a.k.a King of Dancehall ni miongoni ya wasanii wachache kutoka Jamaica walioweza kutoboa anga na kuliteka soko la muziki la Marekani… umaarufu wake Marekani ulisukuma jina la Sean Paul kuvuka mipaka mikubwa zaidi na kugusa masikio ya watu wengi wa sehemu mbalimbali duniani na miondoko yake ya Dancehall Music.
Inawezekana unafahamu vingi kuhusu staa huyu wa muziki wa Dancehall lakini leo nataka nikusogeze kitu kimoja tu cha kufahamu kuhusu Sean Paul… je unajua ni nani aliyemsukuma Sean Paul kuupeleka muziki wake Marekani?!
Nimekutana na interview aliyofanya staa huyo siku chache zilizopita, na ndani aligusia stori iliyomsukuma kuangalia fursa atakayoweza kuipata ikiwa tu atausogeza muziki wake kwenye soko kubwa la muziki duniani, Marekani…
>>> “Kati ya watu muhimu maishani mwangu, siwezi kusahau kumtaja Busta Rhymes. Busta amekuwa mwalimu, mshauri, rafiki na ndugu yangu kwenye vitu vingi sana hasa kwenye biashara ya muziki…. yeye ndiye aliyenifundisha styles fulani za muziki amabazo kwa kipindi hicho Jamaica tulikuwa bado hatuzifanyi na pia alifundisha jinsi ya kuzitumia style hizo kuboresha muziki wangu… baada ya muda akanitafuta na kunishauri sana kuupeleka muziki wangu Marekani, kwani aliamini utanifungulia njia kubwa sana lakini baada ya kusita kwa muda nikaona ngoja nijaribu bahati yangu… baada ya hapo kila kitu kikaniyookea, na pengine asingenisukuma leo nisingekuwa na jina kubwa sana…” <<< Sean Paul.
Kingine alichogusia Sean Paul kwenye interview hiyo ni ujio wa album yake mpya ambayo staa huyo amesema itakuwa mtaani mwaka 2016.
Kipindi hicho mwaka 2002 wakati goma hii inabamba ulikuwa wapi mtu wangu?
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.