Headlines za uhamisho wa rekodi wa Raheem Sterling kutoka Liverpool kwenda Man City wenye thamani ya pound milioni 49 sambamba na mshahara wa pound 180,000 uliingia katika headlines. Uhamisho huo ulimuweka Sterling katika rekodi ya kuwa mchezaji mwenye thamani zaidi wa Uingereza ila kinachovutia sasa ni gari yake anayotumia.
Sterling analipwa mshahara wa pound 180,000 kwa wiki ambazo ni zaidi ya milioni 300 za kitanzania, hivyo kutokana na mshahara huo wengi walitegemea kumuona Sterling akitembelea gari lenye thamani kubwa kama walivyo mastaa wenzake wa Man City ambao wanatembelea magari ya kifahari na yenye thamani kubwa.
Ni kawaida kwa Sterling kumuona akienda mazoezini na Range Rover au Mercedes ila gari aliloonekana nalo December 10 akienda mazoezini aina ya Smart Fortwo Grandstyle linauzwa pound 12,000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 35. Kabla ya uhamisho wa poundi milioni 49 ambao ulimfanya Sterling kuvuta mshahara zaidi ya mara tatu ya aliokuwa analipwa Liverpool aliongea maneno haya.
“Sitaki kuzungumza sijui magari mangapi ya kifahari nitaendesha, kiukweli ninachotaka ni kuwa bora kadri ya uwezo wangu” >>> Raheem Sterling, kauli ya Sterling ya kutokuwa na mipango ya kununua magari ya kifahari zaidi, imeanza kuthibitika baada ya staa huyo kuanza kutembelea gari la Smart Fortwo Grandstyle.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.