November 2 shirikisho la soka barani Afrika CAF limetangaza majina 1o ya wachezaji soka wanaowania tuzo ya mchezaji bora Afrika sambamba na majina ya wachezaji 10 wengine wanaowania tuzo hiyo kwa wachezaji wanaocheza Ligi za ndani ya Afrika.
December 14 shirikisho hilo limechuja majina hayo 20 ya wachezaji waliokuwa wanawania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza Ligi za ndani ya Afrika na wachezaji wanaowania tuzo hiyo ya Afrika kwa ujumla, mchujo uliyofanywa na CAF umepelekea kupatikana kwa majina matatu kwa kila upande.
Majina yaliyotajwa kwa wachezaji wa ndani ya Afrika ni Mbwana Samatta mtanzania anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Robert Kidiaba golikipa wa TP Mazembe na timu ya taifa ya Kongo na Baghdad Bounedjah wa Algeria anayekipiga katika klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia.
Lakini kwa upande wa wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa ujumla ni kiungo wa mitaifa wa Ivory Coast na klabu ya Man City ya Uingereza Yaya Toure, Pierre – Emerick Aubameyang kutoka Gabon na klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani na Andre Ayew wa Ghana lakini anakipiga katika klabu ya Swansea City ya Uingereza. Tuzo hizo zitatolewa January 7 2016 Abuja Nigeria.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.