Headlines za golikipa mkongwe ambaye amewahi kucheza katika vilabu vya Simba na Yanga pamoja na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Ivo Mapunda kuhusu suala la umri wake na lini atastaafu soka limeingia katika headlines kwa mara nyingine tena baada ya wengi kuona ameajili na Azam FC kwa mkataba wa muda mfupi, hivyo huenda wakatarajia anakaribia kustaafu.
Ivo Mapunda ambaye amecheza soka kwa muda mrefu katika vilabu vya Yanga,Simba, St George ya Ethiopia, Bandari na Gor Mahia za Kenya, amejibu stori za yeye kuhusu lini atastaafu, Ivo amejibu kuwa mpango wa kustaafu leo wala kesho haupo katika akili yake labda baadae kama atafikiria ndio atajua.
“Nimepokea vizuri maamuzi ya Azam ya kunisajili kwani nitajifunza vitu vingi kutokana na Azam kuwa na wachezaji wa kimataifa, hata kama ningeenda nje ya nchi ningekutana na wachezaji wengine, nina mkataba wa mwaka mmoja na Azam, kuhusu kustaafu soka sitarajii na sijui lini namtegemea mungu nadhani nitafanikiwa” >>> Ivo Mapunda
Kwa sasa Ivo ana mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Azam FC baada ya kujiunga na timu kama mchezaji aliyeomba kufanya mazoezi ila baadae kocha Stewart Hall alivutiwa na uwezo wake na kuushawishi uongozi wa Azam FC kumsajili na kufuta mpango wa golikipa huyo aliyekuwa anajiandaa kutimkia klabu ya AFC Leopard ya Kenya.
Sauti ya Ivo Mapunda
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.