Baada ya uchnguzi wa kina kufanyika na wachunguzi wa shirikisho la soka ulimwenduni FIFA wameamua kutoa adhabu ya kuwafungia miaka nane kutojihusisha na masuala ya soka aliyekuwa Rais wa soka ulimwenguni FIFA Sepp Blatter na Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya Michel Platini.
Blatter na Platini wamekumbana na adhabu hiyo baada ya kukutwa na hatia ya kufanya matumizi ya fedha kinyume na taratibu. Blatter anatuhumiwa kufanya malipo ya milioni 2 za Uswiss mwaka 2011 kwenda kwa Platini kama Rais wa FIFA malipo ambayo ni kinyume na taratibu na ameshindwa kuthibitisha zilitumika kufanyia nini.
Blatter mwenye umri wa miaka 79 amefungiwa miaka nane kutojihusisha na masuala ya soka sambamba na faini ya 50,000 za Uswiss kutokana na kushindwa kuheshimu sheria za FIFA, wakati Platini amepigwa faini ya 80000 za Uswiss kutokana na kuhusika katika mchakato huo.
“Samahani yangu binafsi kwa FIFA na kwa mchezo wa mpira wa miguu, nitapambana kwa ajili yangu na FIFA, nafungiwa miaka nane kwa kosa lipi? Nitakutana na mwanasheria wangu kujadili kipi sahihi na kipi sio sahihi na kipi ni haki. Tutakata rufaa tena” >>> Blatter
Video ya Blatter akizungumza baada ya hukumu hiyo kutoka
https://youtu.be/bVAmoA5_kEY
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.