Ikiwa ni siku 13 zimepita toka Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli atangaze baraza lake la mawaziri, kwa siku 13 toka Nape Nnauye apate dhamana ya kuwa waziri wa michezo, sanaa na utamaduni, amemaliza mgogoro ambao huenda ungeiua Stand United na fedha za udhamini kupotea bila sababu za msingi.
Baada ya headlines nyingi kuandikwa kuhusu mgogoro uliopo ndani ya klabu ya Stand United chama la wana, December 23 waziri wa michezo Sanaa na utamaduni Mheshimiwa Nape Nnauye ametangaza rasmi kumaliza mgororo huo baada ya kumuagiza mkuu wa mkoa wa Shinyanga kuvunja timu ya muda iliyokuwa imeundwa ili kuangalia matumizi ya fedha za udhamini.
“Timu ya Stand United iliomba kuja kuniona waziri wa michezo na kutatua migogoro yao, kwa historia ya hiyo timu imeanzishwa na vijana wa Stand Shinyanga kwa kuchangishana hadi wakapanda daraja, ila baada ya kutokea udhamini wa ACACIA, kukaibuka migogoro kati ya viongozi wa zamani na timu ya muda ya kuwasaidia iliyoundwa na ofisi ya mkuu wa mkoa, wizara imeamua timu ya mkuu wa mkoa ivunjwe na wajiendeshe wenyewe” >>> Nape Nnauye
Kama utakuwa unakumbuka vizuri mwezi July 2015 kampuni ya ACACIA ambayo inajishughulisha na biashara ya uchimbaji na utafutaji wa madini, ilitangaza kutoa udhamini wa miaka miwili wenye thamani ya zaidi ya bilioni 2 za kitanzania kwa klabu ya Stand United ya Shinyanga, fedha ambazo ndio zilikuwa zinaleta mgogoro wa kiutawala.
Unaweza kusikiliza dakika 2 za Nape Nnauye hapa mtu wangu
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.