Ni stori iliyoanza kuchukua headlines kuanzia Dec 23 ambapo mkongwe wa muziki, Afande Sele alipohojiwa na mtandao maarufu na kusema ‘Wanaoenda kushoot South wana biashara za siri’ kauli hiyo imeonesha kumkera Madee ambaye alimtaka aombe radhi kwa wasanii wenzake.
‘Unajua yale ni matusi kwenye muziki kwenye Bongo Fleva halafu watu kama Afande Sele ndio waanzilishi wa huu muziki sasa muziki unapoelekea sasa ni kwenye level ya kimataifa muziki unakua kwahyo vitu alivyokuwa anafanya yeye mwanzo..kwasasa anaviona vipya anaona kama maajabu watu kumiliki hela nyingi…astaajabu na kuhisi labda wasanii wanafanya ishu nyingi‘ – Madee
Kadri unavozidi kukua na ndio akili zinarudi utotoni… pic.twitter.com/hR4sKAXmtp
— Madee (@Madeeseneda) December 23, 2015
‘Anazungumzia suala la wasanii kushoot nje ya nchi Labda tuchukulie mfano John Legend alipotoka kwao Marekani ambapo kuna vitu vingi na kuja Zanzibar kushoot video yake Je alikuja kufanya vitu vya siri eeeh! Hii ni katika harakati za kutanua wigo wa muziki, watu wanataka kufanya vile vitu ambavyo hatukuwahi kufanya ili twende sawa na soko la kimataifa’ -Madee
‘Sasa wewe Baba au Babu yetu ambaye unastaajabu kuona watu wanatoka kwenda kushoot sehemu nyingine wewe unasema wanaenda kufanya vitu vya ajabu unakuwa unatukatisha tamaa sisi ambao tumeachiwa hii nafasi kwahiyo nikiwa kama msanii namuomba Afande Sele awaombe radhi wasanii wote kwa ujumla kutokana na kauli yake aliyoizungumza sio nzuri’ – Madee