Kama ulipitwa na stori kubwa tatu kwenye 255 iliyosikika kwenye show ya XXL Clouds FM, ninazo hapa za Joh Makini, Diamond na Afande Sele.
Joh Makini kwenye level za kimataifa sasahivi… rapper huyo amesema kuna majina makubwa ya wanaotaka collabo ila hawezi kuyataja japo kwenye majina hayo yupo Davido pia kutoka Nigeria.
Nahreel aliwahi kuzungumzia kuhusu kutosikika sign ya ‘Nahreel on the beat‘ kwenye mdundo wa ‘Nana‘… leo kapatikana Diamond Platnumz ambaye amesema copy ya wimbo wa kwanza kabla ya kufanyiwa mastering ndiyo iliyotumika kwenye video na director wa video Godfather… ilipotokea Nahreel kaifanya nyingine inayomtaja Nahreel, director wa video hakuwa tayari kupokea copy hiyo ya wimbo wa ‘Nana‘ ambayo imeongezewa kipande hicho kwa sababu isingefit kwenye dakika za wimbo ulivopangwa.
Afande Sele amesema alianza kutumia jina la ‘Simba‘ tokea mwaka 2000, aliwahi kuachia ngoma akajiita ‘Simba Dume‘, kwa hiyo kama Blue na Diamond wanajiita ‘Simba’ yeye yuko tayari wakutane na ifanywe ngoma kwa pamoja kila mmoja ajielezee ni simba wa aina gani.
255 ns stori zote hii hapa mtu wangu
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE