Staa wa kimataifa wa Argentina anayekipiga katika klabu ya Manchester City, Sergio Kun Aguero amekiri kuwa angependa kumuona mshambuliaji wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi akijiunga na Manchester City japokuwa anaamini sio rahisi kufanya uamuzi huo.
Ni zaidi ya mara mbili Lionel Messi anahusishwa kuhitajika na Man City, hata siku za hivi karibuni kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini, amekuwa akihusishwa kumuhitaji staa huyo wa FC Barcelona ili aje kuitumikia klabu hiyo ya Ligi Kuu Uingereza.
“Ni vigumu sana kwa Messi kuondoka Barcelona kwasababu alichezea hapo tangu utotoni, na sio rahisi kwake kufikiria timu nyingine ya kuchezea. Hivyo sina matarajio kama anaweza akajiunga na Man City, lakini ni maamuzi ya mchezaji mwenyewe, na nadhani anajisikia vizuri kuwa na Barcelona”>>>Aguero
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.