Maamuzi haya yalikuwa yakisubiriwa na wengi Dar es Salaam, na kwa sababu Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam iliahidi kwamba maamuzi yanatoka leo, macho na masikio ya wengi yalielekea huko kwa siku nzima.
Zoezi la bomoabomoa lilianza mwishoni mwa 2015, likasimamishwa kwa muda alafu taarifa ikatoka kwamba zoezi litaendelea leo Januari 5 2015, lakini kwa upande wa walioenda kupeleka pingamizi Mahakamani pia maamuzi yametoka leo.
Mahakama Kuu Dar es Salaam imeagiza zoezi la bomoabomoa lisimamishwe kwa nyumba 764 ambazo nyingine tayari ziliwekwa alama ya ‘X’… Mahakama imesema shauri la nyumba hizo liko Mahakamani kwa sasa.
#MillardAyoUPDATES: Mahakama Kuu Dar yasitisha bomoabomoa nyumba 764, kwa zilizojengwa mabondeni na maeneo ya wazi yaagiza zoezi liendelee.
— millard ayo (@millardayo) January 5, 2016
Kingine ni kwamba Mahakama hiyo imeruhusu Serikali kuendelea na bomoabomoa kwenye maeneo ambayo ni hatarishi kama mabondeni na maeneo ya wazi.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.