Michuano ya Kombe la Mapinduzi iliendelea leo January 5 katika uwanja wa Amaan kama kawaida, mchana wa January 5 ulipigwa mchezo wa tano wa Kombe la Mapinduzi na watatu kwa Kundi B lenye timu za Yanga, Azam FC, Mtibwa Sugar na Mafunzo ya jeshi la magereza visiwani Zanzibar.
Mchezo wa mchana wa January 5 ulizikutanisha timu ya Mafunzo ambayo mechi yake ya kwanza ilifungwa na Yanga goli 3-0 na Mtibwa Sugar ambayo ilitoka sare ya goli 1-1 na Azam FC katika mchezo wa kwanza, mchezo kati ya Mafunzo dhidi ya Mtibwa Sugar ulilazimika kwa Mtibwa Sugar kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
Mtibwa walianza kwa kucheza soka la taratibu na kipindi cha kwanza dakika ya 12 kupitia kwa Said Bahanuzi walifanikiwa kupata goli la kwanza, goli ambalo lilidumu kwa dakika zote 90. Kwa matokeo hayo Mtibwa watakuwa wanaongoza Kundi B wakiwa na point nne, huku wakisubiri matokeo ya mchezo wa Yanga dhidi ya Azam FC utakaochezwa usiku.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.