Wakenya wameanza mwaka wa 2016 kwa kuomba Watanzania waondolewe kwenye mtandaoa wa Instagram, mtandao maarufu wa kijamii!
Watumiaji wa mtandao huo kutoka Kenya, wanadai Watanzania wamethibitisha kuwa hawawezi kutumia mtandao huo vizuri kutokana na lugha nzito inayotumiwa na Watanzania pamoja na tabia ya baadhi ya Watanzania kupost videos za utupu kwenye mtandao huo.
Wakenya wengi wanadai video hizo zinatangaza vitu visivyopendeza ikiwa kuchochea tabia ya ngono kwenye mtandao huo kitendo ambacho kinawakwaza Wakenya wengi wanaodai kuwa mambo hayo huleta picha mbaya pamoja na kuchafua jina la East Africa.
Hizi ni baadhi ya Posts za watumiaji wa Instagram kutoka Tanzania zilizowagusa Wakenya kwa undani…
Na kupitia hizi tweets chache nilizofanikiwa kuzinasa, huu ndio mjadala unaoendelea chini ya hashtag #KickTanzaniansOutOfIG kwenye Twitter…
>>> “ Kabla hujaniamba #KickTanzaniansOutOfIG, tunaweza tukatokomeza ujinga kwenye mitandao ya kijamii? Kuna sababu UNFOLLOW ipo, itumie vizuri.“<<< @Baba Joy.
>>> “Kabla ya #KickTanzaniansOutOfIG hakikisha mnawafukuza hao viongozi wenu ambao ni mafisadi kwenye Serikali yenu.” <<< @Adamprince.
>>> “Kama wangekuwa makini sana kutokomeza ukabila nchini mwao kama walivyo makini ku-#KickTanzaniansOutOfIG….” <<< @Semkae.
>>> “ Watanzania wakiwa wanafikiria kwa nguvu namna ya kutumia msamiati wa KISWAHILI #KickTanzaniansOutOfIG.” <<< @KOTnewsAt9.
>>> ” Hii ina maliza kila kitu..#KickTanzaniansOutOfIG.” <<< @Ero Kisemei.
>>> “Naona hii hashtag #KickTanzaniansOutOfIG tuifanye kupitia sms maana hakuna Watanzania kwenye Twitter” <<< @Benjah.
>>> “ #KickTanzaniansOutOfIG Kwahiyo tutawafukuza Watazania IG kupitia Twitter. Sawa….” <<< @Neshkev.
>>> “ @Neshkev umena. Ujinga mwengine wa Wakenya unashangaza. Tanzania ni ndugu zetu period! Wakitoka na sisi tutatoka hatupo juu yao.” <<< @kenakadogo.
>>> “ Time Line yangu…. haswa kwa wale wenye hashtag #KickTanzaniansOutOfIG… nyingi hazichekeshi!!!” <<< @suavearnold.
>>> “#KickTanzaniansOutOfIG wakati huohuo kwenye IG #IStandWithTanzanians…” <<< @Ramgeedavis.
>>> “Hawa Watanzania wanafanya IG eneo hatarishi, nendeni mkawa-unfollow….” <<< @BryanJuma.
>>> “#KickTanzaniansOutOfIG Kumfollow Mtanzania ni kitendo cha aibu kwenye Instagram!” <<< @XtianDela.
>>> “Sikujua Watanzania wana Instagram mpaka pale nilipoona #KickTanzaniansOutOfIG“. <<< Lord Mikel.
>>> “#KickTanzaniansOutOfIG wanapenda kuacha namba zao za WhatsApp kwenye kila picha ya mrembo” <<< @Ms.Kiyiekah.
>>> “#KickTanzaniaOutOfIG Watanzania wanashare sana vitu vya utu uzima ambavyo vimeanza kuonekana kwenye feeds za Wakenya. Tunahitaji kusitisha hili.” <<< @XtianDela.
Kama una chochote cha kusema juu ya suala hili, share na mimi hapa chini kwenye comment.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE