Good news ni kwamba yale mabilioni ya elimu bure ya rais Magufuli tayari yameshawafikia watu wangu wa Mwanza….Kazi inabaki kwako mtu wangu kuhakikisha mwanao nae anayatumia kwa ufasaha ili ajikwamue baade, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo ndio mwenye uthibitisho kamili; – Mkuu wa mkoa Mwanza Magesa Mulongo
‘Kwa upande wa sekondari kwa mkoa wetu tuna jumla ya sekondari 197 kwa ujumla wake mkoa kupitia shule za sekondari kwenye akaunti zao za shule wamepokea milioni 642,648,000…ndani ya fedha hizi kuna fedha ya ruzuku, fidia ya ada za kutwa na bweni pamoja na chakula kwa shule za bweni kwa wilaya zetu zote na mkoa mzima, nimatumizi ya mwezi January serikali itaendelea kutoa fedha kila mwezi unaohusika;-RC Magesa Mulongo
‘Kwa upande wa shule za msingi tuna jumla ya shule 850 katika mkoa wetu, hizi nazo tarehe 30 December 2015… akaunti zote za shule za msingi kwenye wilaya na mkoa wetu wote ziliingiziwa kiasi cha shilingi milioni 356,728,000…Fedha ya chakula na ruzuku, kwa hiyo kwa ujumla wake hii ndio fedha ambayo tayari imeshatolewa kama ambavyo serikali iliahidi; – RC Magesa Mulongo
‘Maafisa elimu na wakuu wa shule wanatakiwa kuhakikisha matumizi halali na sahihi ya fedha hizi..Kila mwezi tutaendelea kufanya ufuatiliaji kabla ya kuingiza fedha nyingine, mbele tutakuwa wakali sana kwa wazazi watakaoshindwa kuwapeleka watoto wao shule; – Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mgesa Mulongo
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.