Staa wa hit singles kadhaa Bongoflevani, Shetta amealikwa kwenye show ya ‘Leo Tena’ radio Clouds FM… kama kawaida, kwenye story moja mbili jamaa akagusia pia Hekaheka aliyowahi kukutana nayo.
Shetta amesimulia kwamba kuna siku aliaga anaenda kwenye mishemishe zake, mama Qayllah nae akaaga anatoka… Shetta akiwa ametulia zake kona hivi na mrembo mwingine, akatokea mama Qayllah… Shetta anasema alijitahidi kuzuga lakini vitu havikwenda sawa.
Mama Qayllah na mrembo huyo aliyetaka kuchepuka na Shetta walirushiana maneno, ukazuka utata alafu baadae Shetta akaondoka na Mama Qayllah wake.
Hekaheka na stori za Shetta kwenye ‘Leo Tena‘ ziko kwenye hii sauti mtu wangu.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.