Usiku wa January 11 Staa wa Barcelona Lionel Messi aliandika historia nyingine baada ya kushinda tuzo ya Ballon d’Or kwa mara ya tano akiwashinda wapinzani wake Cristiano Ronaldo pamoja na Neymar.
Mashabiki wa Cristiano Ronaldo katika mji wa Madeira alipozaliwa staa huyo hawakufurahishwa na ushindi wa Messi..walichofanya waliamua kwenda kwenye sanamu lake lililopo katikati ya mji na kuanza kulichafua kwa kuandika jina la Messi.
Mashabiki hao walichafua sanamu hilo lililowekwa mwaka 2014 kwa kutumia rangi nyekundu wakiandika jina lake pamoja na namba 10 ambayo imekuwa ikitumiwa na Messi kama ishara ya kuchukizwa na kushindwa kwa staa wao Ronaldo.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na MillardAyo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.