Fainali ya 10 ya michuano ya Kombe la Mapinduzi imemalizika visiwani Zanzibar, kwa kuzikutanisha timu za Mtibwa Sugar ya Tanzania dhidi ya klabu ya URA ya Uganda. Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Amaan ulichezwa ukiwa na presha ya kawaida kutokana na idadi ya mashabiki kuwa ya kawaida.
Mchezo ulianza kwa Mtibwa Sugar ya Tanzania, kuanza kwa kucheza mpira mzuri, lakini URA walionekana kucheza kwa nidhamu, kwani dakika ya 16 kipindi cha kwanza Julius Ntambi alipachika goli la kwanza kwa URA lililopelekea Mtibwa kurudi kipindi cha pili wakiwa na presha kubwa ya kutaka kusawazisha goli hilo.
Kipindi cha pili URA walionekana kuwa makini na kucheza kwa tahadhari, kwani Mtibwa walikuwa hawakauki golini kwa URA kusaka goli la kusawazisha, wakati mashabiki wakiwa na imani kubwa Kombe hilo kubaki Tanzania kwa Mtibwa Sugar kusawazisha, Peter Lwassa akitokea benchi alikuja kupachika goli la pili dakika ya 85 ns 88 akaongeza la tatu lililofanya mashabiki wa Mtibwa waanze kutoka uwanjani.
Kujiamini kupita kiasi kwa URA kuliwafanya Mtibwa Sugar kupata goli la kufutia machozi dakika ya 90, baada ya Jafari Salum kumpora mpira kipa wa URA Brian Bwete na kupachika goli la kufutia machozi na kufanya mchezo umalizike kwa URA kuibuka na ushindi wa goli 3-1. Hii ni fainali ya pili ya Mtibwa Sugar kupoteza, baada ya mwaka jana kupoteza dhidi ya Simba.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.