Moja ya ripoti kubwa siku ya leo inahusu ishu ya matokeo ya mtihani wa kidato cha pili uliofanyika mwaka 2015, matokeo yako tayari na inaonesha asilimia kubwa ya wanafunzi wamefaulu.
Ripoti hiyo na matokeo inaonesha jumla ya wanafunzi 324,068 wamefaulu mtihani huo kati ya 363,666… kwa hesabu nyingine ni kwamba waliofaulu ni 89% kati ya wanafunzi wote Tanzania.
Hongera pia ziende kwa mikoa ambayo imeingia 10 bora mwaka huu ikiwemo Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya na Iringa pia.
#MillardAyoUPDATES: NECTA yatangaza matokeo ya kidato cha pili 2015 waliofaulu ni 324,068 sawa na 89%, Dar, Mwanza, Mbeya zaingia kumi bora
— millard ayo (@millardayo) January 15, 2016
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.