Katika maisha watu hupitia njia mbalimbali ili kuweza kufikia malengo katika maisha yao, wengine huwa wanapangiwa na wazazi wao kazi ambazo wangependa watotot wao wafanye, lakini wengine uchagua wenyewe, January 18 mtu wangu wa nguvu nakusogezea exclusive interview ya millardayo.com na mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya anayeichezea klabu ya Azam FC Alan Wanga.
Kama ulikuwa hujui huu ni upande wa pili wa maisha ya Alan Wanga, mama mzazi wa mshambuliaji huyo ambaye pia amewahi kuichezea klabu ya Al-Merreikh ya Sudan, ambaye kwa sasa ni marehemu alitaka Wanga awe askari jeshi au mwalimu na sio mchezaji soka kama ambavyo alivyo sasa.
Mama yake mzazi Wanga alimfanyia Alan mipango ya kwenda kujiunga na mafunzo ya jeshi ili awe mwanajeshi, mipango ambayo kama ingefanikiwa Wanga asingekuwa mwanasoka na kama angecheza soka basi katika timu za majeshi kama Ulinizi FC ya Kenya, mipango ya Wanga kujiunga na jeshi ilikwama baada ya wazazi wa staa huyo kushindwa kulipa hela yaani rushwa ili Wanga achaguliwa, licha ya kuwa majaribio alifuzu.
“Mama yangu alitaka niwe mwalimu au mwanajeshi, kwani alikuwa haamini kama mpira unaweza kuendesha maisha ya mtu, ila baba alikuwa ananisapoti sana, kwani amewahi kucheza soka hadi timu ya taifa, mama alikuja kunisapoti wakati nilipopata nafasi ya kujiunga na Tusker FC ndio akaamini kuwa naweza fanikiwa, niliwahi kufanya majaribio ya kujiunga na jeshi na kufuzu ila wazazi walishindwa kutoa rushwa” >>>Alan Wanga
Unaweza msikiliza hapa
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.