Jumapili ya January 24 klabu ya Dar Es Salaam Young African ilishuka dimbani kucheza mchezo wake wa Kombe la FA dhidi ya Friends Rangers, lakini huu ulikuwa ni mchezo wa kwanza kwa kiungo wa kimataifa wa Rwanda anayeichezea klabu hiyo Haruna Niyonzima kurejea uwanjani toka amalizane na uongozi kuhusu matatizo yake.
Stori au jambo lililovuta hisia za watu wengi ni kuhusiana na Haruna Niyonzima kutovaa beji ya unahodha ambayo, yeye alistahili kuvaa, badala ya Vicent Bossou kwani ndio nahodha msaidizi, mara nyingi kama Canavaro hayupo yeye huwa anavaa, Amplifaya ya Clouds FM ilifanya exclusive interview na Haruna Niyonzima juu ya suala hilo. Kavuliwa unahodha?
“Siwezi kulizungumzia nimetoka kwenye matatizo kikubwa ni nimerudi kazini, kuhusu mshahara wa nyuma bado sijalipwa ila nitalipwa kwani ipo kwenye mchakato, nikiwa nimetoka kwenye matatizo yangu ni ngumu kuliweka akilini suala la kuwa unahodha, hivyo mwali anaweza kumchagua mchezaji yoyote atuongoze kwani sisi sote ni manahodha na familia moja akivaa yoyote sawa tu” >>> Niyonzima
Hii ni sauti ya Haruna Niyonzima
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.