Uingereza imeingia kwenye rekodi nyingine tangu mwaka 1977 baada ya wachezaji wake wawili wa mchezo wa tennis kufanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali.
Wachezaji hao Johanna Kontana na Andy Murray walivunja rekodi hiyo baada ya kutinga hatua ya nusu Fainali ya mchuano wa tenisi ya wazi ya Australia.
Konta alikuwa wa kwanza kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kumfunga mpinzani wake Zhang Shuai kutoka China kwa seti 6-4 6-1 na sasa atacheza na Angelique Kerber raia wa Ujerumani ambaye anashika nafasi ya 7 kwa ubora duniani huku yeye akiwa nafasi ya 47 katika ubora.
Konta sasa amekuwa mwanamke wa kwanza raia wa Uingereza kufuzu kwenye hatua ya nusu fainali tangu Jo Durie afuzu mwaka 1983.
Kwa ushindi huo Muingereza huyo atajinyakulia kiasi cha pauni £370,000 pia amepanda hadi nafasi ya 30 kwa ubora duniani.
Mwenzake Andy Murray aliingia nafasi hiyo baada ya kumfunga David Ferrer kwa seti 6-3 6-7 (5-7) 6-2 6-3.
Murray sasa atapambana na mshindi kati ya Gael Monfils na Milos Raonic atakayepatikana Ijumaa.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE