Siku kadhaa zimepita toka Azam FC iweke wazi kuwa wako katika maandalizi ya kuelekea Zambia kuweka kambi ya maandalizi ya mechi zao za kimataifa kwa kucheza mechi kadhaa za kirafiki na kujiweka sawa, hivyo waliiomba bodi ya Ligi hiarishe baadhi ya michezo yao ya Ligi na kwenda Zambia.
Kufuatia mpango huo uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu hiyo Haji Manara hawaungi mkono maamuzi ya TFF na wanaomba TFF kutoa sababu za msingi kwa vilabu vyote ili vijiridhishe.
“Mkisoma kanuani ya 9 inayozungumzia kuahirishwa kwa Ligi, kipengele A kinasema timu itakapo kuwa na wachezaji watano au zaidi katika kikosi cha timu ya taifa inaweza kuhairishwa mechi yao, kwa sasa hakuna timu ya taifa hivyo Azam FC kipengele hicho haikihusu, kipengele B kinasema kuwa lazima timu iwe inacheza mechi za mashindano za kimataifa na taarifa itoe siku 14 kabla, kitu ambacho na uhakika Azam FC hawakufanya, TFF inawaruhusu kwa kigezo gani” >>> Manara
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.