January 27 2016 kikao cha Bunge kimeendelea Dodoma, yakaanza maswali na majibu kwa Mawaziri wa Serikali… baadae Waziri Nape Nnauye akatangaza kwamba kumekuwa na gharama kubwa sana TBC1 kurusha Live kikao cha Bunge kwa hiyo Bunge halitoendelea kurushwa, litarekodiwa na kurushwa usiku.
Hoja ya Waziri ikapelekea baadhi ya Wabunge kuamua kutoa hoja zao wakisisitiza kwamba hawakubaliani na suala hilo, Bunge likaahirishwa.
Bunge likaanza tena saa kumi jioni na baadhi ya Wabunge wakaendelea na msimamo wa kutotaka hoja ya TBC1 kutorusha matangazo ya Bunge Live, ikabidi Askari waingie ndani kutuliza hali hiyo.
Hapa ni Tweets alizoandika Mbunge Zitto Kabwe baada ya kutokea hali hiyo.
TBC walikuwa na fedha ya kurusha hotuba ya Rais ‘live’ ila hawana fedha ya kurusha mjadala wa hotuba hiyo!… https://t.co/9tUhbQRGva
— Zitto Kabwe Ruyagwa (@zittokabwe) January 27, 2016
Kuna wanaouliza, USA wanaonyesha Bunge ‘live’? UK je? Ifahamike kuwa Nchi hizo mabunge yao yana TV na yanarusha… https://t.co/duQVEadlEb
— Zitto Kabwe Ruyagwa (@zittokabwe) January 27, 2016
Hoja ya gharama ni hoja dhaifu sana katika kuzuia mikutano ya Bunge kurushwa ‘live’. Demokrasia ni gharama
— Zitto Kabwe Ruyagwa (@zittokabwe) January 27, 2016
Policemen, in uniform and commandos in plain cloths, were sent into the house and forcefully took legislators out. Never witnessed this
— Zitto Kabwe Ruyagwa (@zittokabwe) January 27, 2016
‘Polisi na makomandoo wameingizwa ndani ya Bunge na kuwatoa Wabunge nje kwa nguvu. Sijawahi kuona kitu kama hiki‘ >> @zittokabwe
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE