Ninazo update mbili mpaka sasahivi mtu wangu, kwanza ni kutoka kwenye kikao cha Bunge Dodoma na nyingine kuhusu ajali ya kivuko kilichozama mto Kilombero.
Kutoka Dodoma >> Baadhi ya Wabunge wametoka nje ya Bunge baada ya Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson kuzuia Wabunge wasiendelee na kuomba mwongozo, Wabunge hao wakaamua kutoka huku Bunge hilo likiendelea kujadili hotuba aliyotoa Rais Magufuli wakati wa ufunguzi wa Bunge hilo.
#MillardAyoUPDATES: Baadhi ya Wabunge wametoka Bungeni baada ya Naibu Spika Dk. Tulia ACKSON kugomea mwongozo ulioombwa na Mbunge.
— millard ayo (@millardayo) January 28, 2016
Kutoka Kilombero, Morogoro >> Taarifa kuhusu ajali hiyo zilianza kusambaa asubuhi ya leo January 28 2016, Waziri Jenista Mhagama akatoa ufafanuzi ndani ya Bunge kwamba ni kweli ajali hiyo imetokea, kivuko kimezama kikiwa kimepakia watu na magari.
Kwenye taarifa hiyo Waziri Mhagama amesema watu 30 wameokolewa kati ya watu 31, jitihada zinaendelea kuokoa watu pamoja na mali.
#MillardAyoUPDATES: Kivuko cha Kilombero kimezama jana usiku kikiwa na magari na abiria, watu 30 wameokolewa kati ya 31, uokozi unaendelea.
— millard ayo (@millardayo) January 28, 2016
Picha za ajali >> Michuzi Blog
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.