Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea tena leo February 4, klabu ya JKT Ruvu ambayo inatumia uwanja wa Karume kama uwanja wake wa nyumbani iliikaribisha klabu ya wagonga nyundo wa jiji la Mbeya, klabu ya Mbeya City kucheza mchezo wake wa 17 wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2015/2016.
Mbeya City imekuwa wababe dhidi ya wenyeji wao klabu ya JKT Ruvu, kwani imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1, Mbeya City walianza kupata goli la uongozi dakika ya 23 baada ya Hassan Mwasapili kutumia vyema nafasi aliyoipata. Lakini dakika ya 38 JKT Ruvu walisawazisha kupitia kwa Musa Juma.
Baada ya JKT Ruvu kusawazisha goli, Mbeya City walirudi tena kwa kasi na dakika saba baada kufungwa wakaongeza goli la pili kupitia kwa Yohana Morris, goli ambalo lilidumu kwa dakika zote 90. Kwa matokeo hayo Mbeya City itakuwa imetimiza jumla ya point 17 na imecheza mechi 17 sawa na Mgambo JKT iliyopo nafasi ya 9.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwapia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagramna YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.