Stori ya Wanafunzi wa Tanzania kuvamiwa na kupigwa huku mmoja wa wasichana akivuliwa nguo na kutembezwa barabarani imechukua headline nyingi kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na vyombo vya habari haswa hapa nchini, uzito wa tukio hili umefika bungeni Dodoma, Na hapa Waziri wa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dk. Augustine Mahiga ana haya ya kusema.
“Jana nilitoa taarifa ya awali kuhusu wanafunzi wa Kitanzania walipingwa na msichana mmoja alivuliwa nguo na kutembezwa barabarani nchini India, taarifa tulizozipata ni kweli kitendo kilitokea”
“lilitokea tukio la mwanafunzi wa Kisudani kuzigonga pikipiki tatu na pia kumgonga mama wa Kihindi ambaye alifariki hapohapo, baada ya tukio mwanafunzi huyo akakimbia”
“Wananchi wa India waliamua kuchoma gari hilo, lakini baada ya muda gari jingine lilifuata likiwa na wanafunzi wanne wa Tanzania akiwemo msichana mmoja. Walilisimamisha lile gari na kuwavuta wanafunzi wale kisha kuwapiga na kuchoma gari lao ”
Hatua gani zimechukuliwa hadi sasa? “Tumemweleza Balozi wa India hapa nchini na akachukua hatua ya kuielezea Serikali yake, na hadi sasa watuhumiwa wote wamekamatwa na wamepelekwa Mahakamani. ” Waziri Mahiga
“Pia jana nilieleza kwamba kuna mwanafunzi mmoja alifariki karibu na eneo lilipotokea hilo tukio, taarifa za awali zilikuwa zinatatanisha tukazani kifo chake kinahusishwa na tukio hilo la uvamizi, lakini sio kweli.. Mtanzania huyo alikuwa anaendesha pikipiki akapata ajali na kufariki palepale ”
Unaweza pia kumsikiliza kwenye hii sauti hapa chini
Na hii ndio ripoti ya jana bungeni
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.