February 5 2016 nakusogezea stori ya Gabe Adams kijana mwenye umri wa miaka 17 aliyezaliwa na ulemavu wa mikono na miguu mwenye uwezo mkubwa wa kucheza muziki, mtu wangu wa nguvu nakusogezea pichaz na video zinazo muonesha Gabe Adams akionesha umahiri wake wa kucheza muziki licha ya kuwa ni mlemavu.
Gabe amekuwa kivutio na mfano kwa wanafunzi wenzake wa Davis High School, kutokana na umahiri wake wa kucheza muziki, kutojitenga na kufanya wenzake wavutike kucheza muziki. Hii ni video ikimuonesha Gabe Adams uwezo wake wa kucheza muziki na wenzake.