Kuanzia mwishoni mwa mwaka 2015 msanii wa bongofleva Mo Music mmiliki wa single ya ‘skendo’ hakuwa na furaha kwa sababu alipata taarifa za kushtukiza kutoka Mahakamani Dodoma kwamba anashtakiwa kwa kosa la kushirikiana na mpenzi wake wa zamani kutapeli zaidi ya shilingi milioni 30 za mtu.
Leo February 23 2016 Mahakama ya wilaya Dodoma imemuondolea mashtaka Mo Music aliyekua mshtakiwa wa pili kwenye kesi hiyo ambayo muhusika mkuu ni mpenzi wake wa zamani anaeshtakiwa kwa kutapeli zaidi ya milioni 30 za Mwanaume mwingine ambaye alitajwa kuwa mpenzi wake mpya.
Kwenye Exclusive na millardayo.com Mo Music alisema wanaume huyo baada ya kushtukia mchezo wa kutapeliwa akaamini Mwanamke huyo aliyekua mtangazaji wa Radio, amekua akichukua pesa kwake na kuzipeleka kwa Mo Music (mpenzi wa zamani)
Mo Music amesema kila ambapo amekua akitaka kutoa wimbo mpya Mwanamke huyo amekua akimletea mabalaa japo tayari ameshaachana naye kitambo, kipindi cha nyuma aliwahi kuzusha kwamba anao ujauzito wa Mo Music na mwanamke huyo alilivalia njuga hili swala mpaka likafika kwenye vyombo mbalimbali vya habari na Mo Music akaamini kachafuliwa jina.
ULIIKOSA BARUA YA MTANZANIA JACKIE CLIFF KUTOKA GEREZANI CHINA? TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE