Leo February 29 2016 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Hamisi Kigwangalla ametoa ripoti ya Ugonjwa wa Kipindupindu kwa wiki ya mwisho ya mwezi february pamoja na idadi ya watu waliofariki tangu kuibuka kwa ugonjwa huo.
Waziri Kigwangalla amesema ‘Hadi kufikia tarehe 28 Februari 2016, jumla ya wagonjwa 16, 825 wametolewa taarifa na kati ya hao, watu 258 wamepoteza maisha‘
‘Jumla ya Mikoa 12 nchini iliripoti wagonjwa katika kipindi cha juma moja lililopita ambapo Mkoa wa Mara uliripoti idadi kubwa zaidi ya wagonjwa ambao ni 125, Iringa 64, Mwanza 59, Morogoro 44, Mbeya 29, Dar es salaam 25, Arusha 18, Kigoma 8, Rukwa 6, Simiyu 6 na Singida 2‘
Wizara ina mkakati gani wa wa kudhibiti ugonjwa huu? ‘Wizara inaendelea kutoa rai kwa jamii, Wataalamu na viongozi katika ngazi zote kwamba kila mmoja wetu atimize wajibu wake katika harakati za kuudhibiti ugonjwa wa Kipindupindu‘
Unaweza kuitapa pia full stori kwenye hii video hapa chini…
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FBYOUTUBE