February 29 2016 stori kutokea Mtwara, ilikuwa ni hii ishu ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kumsimamisha kazi mmoja wa Madaktari wa hospitali ya Rufaa ya Wilaya mkoani hapo.
Daktari huyo alituhumiwa kuomba rushwa ya Shilingi laki moja kutoka kwa mgonjwa, hatua hiyo ikampelekea pia Waziri Mkuu huyo kukasirishwa na kuagiza maduka yote ya dawa yaliyokaribu na hospitali hiyo kufungwa mara moja kutokana na madaktari kujihusisha na biashara hiyo na kuachana na dawa za Serikali.
‘Nani alitaka laki moja kutoka kwa mgonjwa?, simama mwenyewe.. ulimuambia kanunue dawa, dawa shilingi 80 unasema kanunue alafu leta laki moja, ameleta dawa unamwambia laki moja yangu iko wapi?’
‘Sasa naanza na wewe, unasimama kazi na uchunguzi uendelee, na wengine wote ntakao wabaini basi utaratibu ni huu‘
Unaweza pia Waziri Mkuu kumsikiliza kwenye hii sauti hapa…
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, InstagramnaYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> n