Jeshi la Polisi Arusha limewaua majambazi watatu waliokuwa wakihusika na matukio ya wizi ambapo lilipovamia kwenye makazi yao, lilikuta milipuko ya mabomu, bunduki, mavazi ya jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) pamoja na ujumbe maalum kwa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Dar es salaam, Suleiman Kova.
Ujumbe uliandikwa ‘Nasaha kwa Kova, Mzee andaa kamati ya mazishi ya vipolisi vyako tukiwamaliza tutakufikia wewe‘
Kamanda wa Polisi Arusha Liberatus Sabas amesema ‘Jeshi la Polisi Arusha lilipata taarifa kuwa kuna mtu wanamuhisi ni mhalifu, tukaweka mtego na kumkamata mtu mmoja, tulipofanya msako katika chumba chake tukakuta milipuko kadhaa‘
‘Alieleza kuwa kuna wenzake anashirikiana nao katika matukio ya ujambazi, usiku majira ya saa 5 Polisi wakiambatana na mtuhumiwa walifika eneo walipokuwa wenzake, baada ya kufika mtuhumiwa alipiga kelele na wenzake wakajua kwamba kuna matatizo ‘
‘Marushiano ya risasi yakaanza na hatimaye Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwajeruhi, jitihada za kuwapeleka hospitali hazikufanikiwa kwasababu watu hao wote walifariki wakati wakipelekwa hospitali ‘
Full stori unaweza kuipata kwenye hii video hapa chini…
FUJO ZILIZOTOKEA UCHAGUZI WA MEYA DAR ES SALAAM KWENYE HII VIDEO HAPA CHINI…
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagramna YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE