Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya Petrol, Diesel na ya mafuta ya taa katika masoko yote ya jumla na rejareja ambapo bei hizo zitaanza kutumika kuanzia Jumatano siku ya pili ya mwezi March 2016.
Mkurugenzi wa huduma za nishati na maji (EWURA), Felix Ngamlagosi amesema >>> ‘kuanzia tarehe 2 March bei za mafuta zimebadilika ikilinganishwa na toleo lililopita la February 2016, kwa March 2016 bei ya rejareja za petroli imepungua Tsh 31 kwa lita sawa na 1.70%, Diesel imepungua Tsh 114 kwa lita sawa na 7.10% na mafuta ya taa yamepungua kwa Tsh 234 kwa lita sawa na 13.75%’
‘kwa kiasi kikubwa , kupungua huku kwa bei za mafuta kwenye soko la ndani kumetokana na kuendelea kushuka kwa bei za mafuta katika soko la dunia‘
Nimekuwekea hapa Orodha ya bei za mafuta kwa mikoa yote
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE