Ishu ya Moshi kutoka soko la samaki Ferry kuingia Ikulu ilichukua vichwa vya habari mwanzoni mwa mwaka huu baada ya moshi huo wa majiko kuwa unaingia mpaka kwenye makazi ya Rais Magufuli (IKULU) na kusababisha kero.
Leo March 8 2016 Mkuu wa wilaya ya Ilala Isaya Mguluni kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, amezindua majiko 48 yanayotumia nishati ya gesi katika soko la samaki Ferry ili kupunguza moshi unaotokana na matumizi ya kuni ambao uliokuwa unaingia mpaka Ikulu.
Awali Mkuu huyo wa wilaya alizindua bodi ya soko la samaki Ferry, ambapo ilikuwa ni kilio cha muda mrefu kukosekana kwa Bodi hiyo tangu kuanzishwa kwa soko hilo, bodi hiyo inaundwa na wajumbe 9 ambao watatekeleza majukumu yafuatayo
- kufanyia kazi mapendekezo ya kamati ya soko
- kutoa miongozo mbalimbali kwa wadau wa soko juu ya taratibu zinazotakiwa kufuatwa ndani ya soko
- kufanya shughuli kwa mujibu wa sheria ndogo hizi
- kuidhinisha mapato na matumizi ya soko (bajeti).
- kusimamia ulinzi na usalama wa soko
- kuthibitisha uteuzi wa mkuu wa soko
ULIIKOSA HII VIDEO WAKATI MOSHI WA FERRY ULIKUWA HAUJAZUIWA KUINGIA IKULU? TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na MillardAyokwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFB YOUTUBE