Leo March 17 2016 headline nyingine ni kutoka kwa Vyama visivyo na uwakilishi bungeni ikiwa ni pamoja na DP, CCK, SAU, AFP, TLP, ADA TADEA, UPDP, D. MAKINI, NRA, UMD, CHAUSTA na ADC vimetoa yao ya kauli yao kuhusu ucchaguzi huo na kusema vitashiriki kwa kufuata sheria ya uchaguzi ya mwaka 1984.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Dar es salaam, Katibu mkuu wa chama cha DP Abdul Mluya amesema ‘Vyama vyetu vianatambua kuwa, chombo chenye mamlaka ya kutangaza tarehe ya uchaguzi kwa mujibu wa sheria ni ZEC na ndio chenye mamlaka ya kumtangaza mshindi aliyeshinda kwa kura nyingi‘
‘Vyama vyetu vimeona kuwa kwa kua vyama hivi vilishiriki uchaguzi kwa nafasi ya Rais oct 25, 2015 vilikuwa 14 vikiwa na imani na tume ya uchaguzi‘ ;-Abdul Mluya
‘kwa imani hiyo ndio maana vyama hivi vilishiriki uchaguzi huo wa awali,hivyo hatunabudi kushiriki uchaguzi huo ili demokrasia ishike mkondo wake na hatimaye mshindi apatikane kwa njia ya kidemokrasia‘ ;-Abdul Mluya
Ilikupita hii video ya Raymond alivyokutana na Diamond Platnumz?
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FBYOUTUBE