Taarifa za hii ajali zilianza kutoka March 19 2016 asubuhi ambapo ndege ilikua na abiria 55 pamoja na Wafanyakazi saba ambapo ilianguka uwanja wa ndege wakati ikijaribu kutua huko kusini mwa Urusi kwenye mji wa Rostov-on-Don ambako hali ya hewa ilikua mbaya.
Wizara ya dharura ya Russia imesema hali mbaya ya hewa ndio inatajwa kuwa chanzo ambapo ilipata ajali kwenye jaribio la pili la kutaka kutua kwenye uwanja huo wa ndege baada ya kuzunguka angani kwa saa mbili ( dakika 120) kabla ya kuruhusiwa kufanya jaribio la pili la kutua.
Wizara hiyo ya dharura nchini Urusi ilishatangaza kwamba kutakua na hali mbaya ya hewa kuanzia March 19 mpaka March 22 2016 ambapo kutoka na ajali hii Fly Dubai na Boeing wametangaza kuanzisha uchunguzi wa ajali hii iliyogharimu maisha ya abiria wote ambao walikua raia wa Russia.
https://www.youtube.com/watch?v=bHaFlx7QVq4
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE