March 21 ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mkali wa soka kutokea Brazil Ronaldinho, ambae kwa siku ya leo anasherehekea kutimiza umri wa miaka 36. Ronaldinho kacheza vilabu kadhaa vikubwa barani Ulaya ikiwemo FC Barcelona. Mtu wangu wa nguvu naomba nikusogezee vitu vitano vya kukumbwa kutoka kwa Ronaldinho.
5- Akiwa na umri wa miaka 13 Ronaldinho aliweka rekodi ya kufunga magoli 23 pekee yake katika mechi moja, rekodi ya Ronaldinho kufunga goli 23 ilimfanya aanze kupata umaarufu akiwa na umri mdogo.
4- Ronaldinho ni miongoni mwa wachezaji wachache duniani waliowahi kushinda mataji yote makubwa ya soka, kama Kombe la Dunia, UEFA, Copa America na mengine mengi.
3- Staa huyo wa Brazil ambae amekuwa maarufu zaidi kutokana skills za kuchezea na kumiliki mpira uwanjani amewahi kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Dunia mara mbili mwaka 2004 na 2005.
2- Ronaldinho bado anatajwa kama mmoja wa wachezaji matajiri zaidi kutokea Brazil, hadi December 20 2014 alikuwa anatajwa kuwa na utajiri wa dola milioni 170.
1- Kama umemiss skills za Ronaldinho unaweza kujikumbusha katika video hii
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na MillardAyo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE