Kulikuwepo na taarifa za baadhi Majengo ya ghorofa jijini Dar es salaam kujengwa chini ya viwango, hali iliyomladhimu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kutoa siku 18 kwa Uongozi wa manispaa ya Ilala kubomoa Jengo la ghorofa 16 lililopo mtaa wa Indira Gandhi.
Kazi hiyo ya ubomoaji alipewa mkandarasi mzawa ambapo ameifanya kazi hiyo kwa siku 47 badala ya siku 90 alizopewa. Akizungumzia zoezi hilo linavyoendelea Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Ilala Isaya Mngurumi amesema…….
>>>’Mchakato wake wa kupata mkandarasi wa kuvunja umechukua zaidi ya miaka miwili, tulikuwa tunategemea wa nje wakagoma, tukachuka wakandarasi wakubwa wakagoma, lakini tukapata mzawa wa ndani ambaye hatukuamini hata sisi lakini amejaribu kufanya kazi yake kwa siku 47, badala ya siku 90. kikubwa alichokifanya ni usimamizi na ufuatiliaji katika suala hili, hakuna mtu aliyekufa wala aliyeumia, ilikuwa ghorofa 16 lakini mpaka sasa hivi kazi imekwisha‘
Kwa upande wake Msimamizi wa ubomoaji Amir Shaban amesema …..>>>’tumefanya kazi kwa usalama zaidi na uangalifu mpaka kazi ilipofikia, sasa hivi tuko kwenye hatua ya kutoa kifusi, ni hatua za mwisho za kazi mpaka tarehe 30 mwezi huu tutakuwa tumeshakabidh kazi‘
Uliikosa video ya mwandishi aliyetekwa Zanzibar na kupatikana Dar na kuongea kwa mara ya kwanza baada ya kupatikana? Angalia video hii hapa chini
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayokwenye Twitter,FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE